Mshambuliaji wa Kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi amewapongeza mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom Simba kwa kufanikiwa kutetea ubingwa wao kwa msimu wa tatu mfululizo
Okwi ambaye kwa sasa anacheza klabu ya Ittihad Alexandria ya nchini Misri, amesema Simba ilistahili ubingwa huo
"Hongereni kwa kushinda ubingwa wa tatu, hakika mlistahili," Okwi aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram

Okwi mwenye heshima ya kipekee katika klabu ya Simba, ameungana na mastaa kibao ambao wametuma salamu za pongezi kwa Simba
Nalo Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) limeipongeza Simba kwa kushinda ubingwa huo
Baada ya mafanikio hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bilionea Mohammed Dewji 'Mo', amesema sasa wanaelekeza nguvu zao kwenye michuano ya kombe la FA na kisha kuanza kuandaa timu kwa ajili ya ligi ya mabingwa msimu ujao