Uongozi wa Yanga huenda ukamrejeshea majukumu yake ya umeneja, aliyekuwa nahodha wake, Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Cannavaro aliyedumu katika kikosi cha Yanga kwa zaidi ya miaka 10, aliamua kustaafu kucheza soka na kupewa cheo cha umeneja wa timu alichodumu nacho kwa takribani mwaka mmoja kabla ya kujiweka kando kwa kile kilichoelezwa kutingwa na masuala ya kifamilia
Hivi karibuni mkataba wake ulimalizika na nafasi yake kuchukuliwa na Hafidh Saleh ambaye pia alikuwa mratibu wa Yanga
Hata hivyo baada ya kuvunjwa kwa benchi la ufundi, mkongwe huyo huenda akajumuishwa kwenye benchi jipya la ufundi litakaloundwa
Kwa sasa Cannavaro ni Meneja wa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ambacho kimeingia kambini juzi kujiandaa na michezo miwili ya kusaka tiketi ya fainali za Afcon 2021