Sasa ni rasmi klabu ya Simba imefanikiwa kutetea ubingwa wake kwa msimu wa tatu mfululizo baada ya kupata matokeo ya suluhu ya bila kufungana dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo uliopigwa uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya
Wekundu wa Msimbazi leo waliingia kwenye mchezo huo wakiwa na lengo moja tu, kutofungwa kwani walihitaji alama moja kuwa mabingwa
Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa nchi Sven Vandenbroeck alifanya mabadiliko makubwa ya kikosi chake akiwapa mapumziko baadhi ya wachezaji kwa ajili ya mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa Jumatano


Simba imefikisha alama 79 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote msimu huu
Miamba hao wa soka nchini, wametwaa ubingwa huku wakiwa na mechi sita mkononi
Huo ni ubingwa wa 21 kwa Simba...!
Hakika ulikuwa msimu mzuri kwa Simba, siku hii ilianza kuonekana mapema tu kutokana na ubora walioonyesha Simba tangu mchezo wao wa kwanza
Hongera Simba kwa kutwaa ubingwa wa tatu mfululizo...!