TAKUKURU yakamilisha kumuhoji Kaburu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
25 Jan 2018
TAKUKURU yakamilisha kumuhoji Kaburu
Upande wa mashtaka katika kesi ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo na kutakatisha fedha inayomkabili, Rais wa Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange, umeieleza mahakama kuwa tayari wameshakamilisha zoezi la kumhoji na kuchukua maelezo ya mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo.

Wakili kutoka Takukuru, Leonard Swai alisema hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa, wakati shauri hilo lilipofikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.

Januari 11, mwaka huu upande wa Mashtaka uliiomba mahakama hiyo kumruhusu mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo, Geofrey Nyage maarufu kama Kaburu, kwenda kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kuhusiana na nyaraka zilizopo katika ofisi ya Aveva.

Mahakama hiyo ilikubaliana na ombi la upande wa mashtaka na kutoa kibali cha kwenda kumhoji mshtakiwa huyo na kisha kumrudisha gerezani.

Hata hivyo, kesi hiyo imeshindwa kuendelea baada ya mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Evans Aveva kuwa mgonjwa na hivyo kushindwa kufika mahakamani.

"Mheshimiwa hakimu, tumeshakamilisha zoezi la kumhoji na kuchukua maelezo ya Nyange kama tulivyoiomba mahakama yako Januari 11, mwaka huu, lakini tumeshindwa kuchukua maelezo ya mshtakiwa wa kwanza ambaye ni Aveva, kwa sababu ni mgonjwa ," alidai Swai na kuongeza

"Mshtakiwa wa pili yupo mbele ya mahakaka yako lakini mshtakiwa wa kwanza (Aveva ) ni mgonjwa na amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akisumbuliwa na tatizo la figo," alidai

Wakili Swai alidai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na kuomba mahakama hiyo kuahirisha shauri hilo.

Awali, upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Nestory Peter akisaidiana na Jailos Mpoki ulidai kuwa kama upande wa mashtaka hawana sababu ya kumhoji mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, wakamilishe upelelezi wao.

Kutokana na maelezo za pande zote, Hakimu Nongwa aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 8, mwaka huu itakapojwa.

Washtakiwa kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka matano likiwemo la kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha USD 300,000, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Katika shtaka la kwanza, washtakiwa hao wanadaiwa kuwa walikula njama ya kughushi fomu ya maombi ya kuhamisha fedha ya Machi 15,2016 wakionesha Klabu ya Simba inalipa mkopo wa USD 300,000 kwa Evans Aveva wakati si kweli.

Katika shtaka la pili alidai kuwa Machi 15,2016 katika benki ya CRDB tawi la Azikiwe Ilala Aveva akijua alitoa nyaraka za uongo ambayo ni fomu ya maombi ya kuhamisha fedha ya Machi 15,2016 wakati akijua ni kosa.

Ildaiwa katika shtaka la tatu la kutakatisha fedha, Aveva na Nyange wanadaiwa kuwa kati ya Machi 15 na Juni 29,2016 Dar es Salaam kwa pamoja walikula njama ya kutakatisha fedha kwa kupata USD 300,000 wakati wakijua ni zao la uhalifu.

Kwa upande wa shtaka la nne la kutakatisha fedha, Aveva anadaiwa kuwa kati ya Machi 15,2016 katika benki ya Baclays Mikocheni alijipatia USD 300,000 wakati akijua zimetokana na kughushi
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Goli la ushindi dhidi ya Fountain Gate; FT : Fountain Gate 0-1 Simba
Goli la ushindi dhidi ya Fountain Gate; FT : Fountain Gate 0-1 Simba
5h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Fountain Gate 1-0 Tanzanite Kwaraa
Simba mwendo mdundo, yaichapa Fountain Gate 1-0 Tanzanite Kwaraa
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Fountain Gate vs Simba, NBC PL, Oct 29
Kikosi : Fountain Gate vs Simba, NBC PL, Oct 29
9h ago
READ MORE β†’
Kamati ya uchaguzi Simba imesisitiza, mchakato unaendelea
Kamati ya uchaguzi Simba imesisitiza, mchakato unaendelea
9h ago
READ MORE β†’
Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
12h ago
READ MORE β†’
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
12h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’