FT : Mbeya City 0-2 Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Jun 2020
FT : Mbeya City 0-2 Simba

Mabingwa wa nchi Simba wamekaribia kutwaa ubingwa wa tatu mfululizo ligi kuu ya Vodacom baada ya kuichapa Mbeya City mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya

Simba iliuanza mchezo huo kwa kasi na ilihitaji dakika tano tu kufunga bao la kwanza kupitia kwa nahodha John Bocco

Krosi murua iliyopigwa na Clatous Chama ilitua mguuni kwa Bocco ambaye bila ajizi aliweka chuma kimiani

Mabingwa hao wa nchi, waliendelea kucheza soka la kibingwa hesabu zikiwa kuondoka na alama zote tatu

Ilikuwa siku nzuri kwa Bocco kwani kwenye dakika ya 55 aliongeza bao la pili ambalo liliihakikishia Simba kuondoka na alama zote tatu

Simba imefikisha alama 78 baada ya ushindi huo na sasa huenda ikahitaji kushinda mchezo dhidi ya Tanzania Prisons ili kutetea ubingwa wake

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’