Achana na shoo kali iliyopigwa na kiungo Said Khamis Ndemla jana, mwamba Gerson Fraga raia wa Brazil ni mmoja wa wachezaji waliofanya vizuri sana kwenye mchezo dhidi ya Mwadui Fc ambao uliishuhudia Simba ikiondoka na ushindi wa mabao 3-0
Fraga amekuwa hapati nafasi mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza, lakini kila anapopata nafasi ya kuanzishwa, huwa anaitumia vyema
Ni bahati mbaya mwamba huyu jina lake huwa halizungumzwi sana lakini pengine kwa kuwa hana vitu vingi sana anapokuwa dimbani
Fraga ni mchezaji anayefahamu majukumu yake vyema katika eneo la kiungo mkabaji
Afisa Habari wa Simba Haji Manara, amemwagia sifa kiungo huyo akibainisha kuwa ni aina ya kiungo mkabaji halisi
"Labda mimi mpira huwa nauangalia tofauti, Gerson Fraga huyu ni kiungo mkabaji halisi, hesabu zake anazipiga sawasawa"
"Kila mara akiwa uwanjani anakaa eneo sahihi,anagongana kisha anapokuwepo umbo laa timu linaonekana, na fikiria huyu katoka nchi ya mbali sana, ukikaa nae zaidi kuna kitu atakupa, binafsi yeye na Ndemla kwa leo walifanya Simba iwe sukari kila eneo," alisema
Fraga yuko ukingoni mwa mkataba wake wa mwaka mmoja na mabingwa hao watetezi, je anastahili kuongezewa mkataba?