Mkwasa awataka wachezaji watambue thamani ya kucheza Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Nov 2019
Mkwasa awataka wachezaji watambue thamani ya kucheza Yanga

Baada ya kuanza majukumu yake kwenye kikosi cha Yanga, kocha Charles Mkwasa amewataka wachezaji kutambua ukubwa na thamani ya kucheza Yanga

Mkwasa amewahakikishia wachezaji kuwa kama watajituma na kujitolea kwa moyo mmoja, hakuna sababu ya timu kutopata matokeo mazuri

"Niwahakikishie wote mlisajiliwa na Yanga kwa sababu mlionyesha ubora na kuwa na sifa ya kuichezea timu hii. Jukumu langu mimi ni kuwasaidia ili muweze kutimiza malengo ya timu," amesema

"Fahamuni mpo hapa kuipigania klabu hii na kubeba vikombe, hilo ndio lengo kuu kwa kila mchezaji anayeitumikia klabu hii"

"Tunapaswa kuishi katika utamaduni huu na ili kutimiza dhamira hii ni lazima tuanze kushinda michezo yetu"

"Tutakaposhinda kila kitu kitarejea katika hali yake, uwanja utajaa na furaha kwa mashabiki itarejea"

Mkwasa ataiongoza Yanga kwenye mchezo wake wa kwanza kesho dhidi ya Ndanda Fc ambao utapigwa uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara

Kikosi cha Yanga kilitua Mtwara jana, leo wanatarajiwa kufanya mazoezi ya mwisho katika uwanja huo

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’