FT : Simba 3-0 Mwadui Fc

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
20 Jun 2020
FT : Simba 3-0 Mwadui Fc

Wakiwa kwenye ubora wa hali ya juu, mabingwa wa nchi Simba wamezidi kuukaribia ubingwa wa tetu mfululizo baada ya kuifumua Mwadui Fc mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa

Simba iliyokuwa bora sana, ilianza mahesabu mapema tu kwa bao safi la kuongoza lililowekwa kimiani na Hassan Dilunga 'HD' ambaye hilo lilikuwa bao lake la saba msimu huu

Baada ya kupata bao la kuongoza, Simba iliendelea kutia presha langoni kwa Mwadui Fc na ilifanikiwa kupata bao la pili, mlinzi wa Mwadui Fc akiijaza kimiani krosi ya Shomari Kapombe

Wakiwa wanafahamu mchezo wa leo ulikuwa muhimu kwao, vinara hao wa ligi walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-0

Bao la tatu lilipatikana kwenye dakika ya 58 likiwekwa kambani na mkongwe, nahodha John Raphael Bocco 'Adebayor'

Katika kipindi cha pili kocha Sven Vandenbroeck alifanya mabadiliko ya wachezaji kwa kuwaingiza Clatous Chama, Meddie Kagere, Francis Kahata, Yusufu Mlipili katika nafasi za Bocco, Dilunga, Miquissone na Kapombe

Ni mabadiliko yaliyoifanya Simba iendelee kutawala mchezo zaidi licha ya kuwa haikuongeza mabao zaidi

Ushindi huo umeifanya Simba ifikishe alama 75 sasa ikihitaji alama 10 kutoka mechi nane zilizobaki

Matokeo ya mechi zote zilizopigwa leo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’