Sven kupangua kikosi mchezo dhidi ya Mwadui Fc

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 Jun 2020
Sven kupangua kikosi mchezo dhidi ya Mwadui Fc

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amefichua mpango wa kupangua kikosi kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mwadui Fc ambao utapigwa keshokutwa Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa

Baada ya ligi kurejea, Simba imeanza kwa kusuasua ikilazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Ruvu Shooting, matokeo ambayo hayakutarajiwa

"Kiukweli kudondosha pointi mbili nyumbani hayakuwa matarajio yetu na shida moja wapo ambayo ilichangia hilo ni wachezaji wangu baadhi kuniangusha jambo ambalo litanifanya kubadili baadhi yao katika mchezo unaokuja"

"Hatuwezi kusema ni kina nani kwani tulicheza kama timu lakini katika mechi na Mwadui utaona baadhi ya mabadiliko ambayo nitayafanya," alisema Sven kwenye mazoezi ya kikosi cha Simba yanayoendelea uwanja wa Mo Simba Arena

Aidha Mbelgiji huyo amesema pia wamesahihisha makosa waliyoyabaini katika mchezo uliopita hivyo kuwa na matumaini ya kufanya vizuri Jumamosi

"Mchezo uliopita tulifanya makosa mengi, tumefanya kazi kubwa kuhakikisha tunayarekebisha hivyo Jumamosi hatutarajii kurudia makosa hayo. Nafikiri tutakuwa na mchezo mzuri ambao utawapa furaha mashabiki wetu," aliongeza Sven

Simba imepania kuondoka na alama zote tatu kabla ya safari ya mkoani Mbeya kuzifuata Mbeya City na Tanzania Prisons

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
5h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’