Klabu ya Yanga itapaswa kumlipa aliyekuwa kocha wake Mkuu Mwinyi Zahera Tsh Milioni 120 baada ya kuvunja mkataba wake, imefahamika
Mpaka jana jioni, Zahera alisema kuwa hakuwa amepokeaΒ barua rasmi ya taarifa ya kuvunjwa kwa mkataba huo
Wengine wanaosubiri kulipwa Mamilioni pamoja na kocha Mwinyi Zahera ni aliyekuwa daktari wa timu Dk Edward Bavu, kocha msaidizi Noel Mwandila, mchua misuli Jackob Onyango, Meneja na Mratibu Hafidh Saleh na Mtunza vifaa Mahmoud Omar
Jana uongozi wa Yanga ulitangaza kulivunja benchi lote la ufundi huku wakimteua kocha na Katibu Mkuu wa zamani wa klabu hiyo Charles Mkwasa kuwa Kaimu kocha Mkuu
Mkwasa atasaidiwa na Said Maulid (SMG) wakati Dismas Ten akiteuliwa kuwa Meneja na Mratibu wa timu
ADVERTISE HERE