Mchezo wa ligi kuu kati ya Simba dhidi ya Ruvu Shooting uliopigwa uwanja wa Taifa, umemalizika kwa timu hizo kugawana pointi baada ya kutoka sare ya bao 1-1
Shiza Ramadhani Kichuya alitangulia kuifungia Simba bao la kuongoza kwenye dakika ya sita kabla ya Ruvu Shooting kusawazisha kupitia kwa Fully Maganga kwenye dakika ya 37
Simba haikuwa na mchezo mzuri sana leo, lakini pia Ruvu Shooting walitoa upinzani kwa mabingwa hao wa nchi

Mchezo unaofuata ni dhidi ya Mwadui Fc na utapigwa Juni 20 hapo hapo uwanja wa Taifa
Kimahesabu, Simba inahitaji alama 13 kuweza kujihakikishia ubingwa wa tatu mfululizo
ADVERTISE HERE