Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck ameeleza kufurahishwa na juhudi anazoonyesha mazoezini na kiungo Ibrahim Ajib ambaye amerejeshwa kikosini jana
Sven amesema anaamini adhabu aliyompa kiungo huyo itamfanya aongeze juhudi na kuwa mchezaji bora zaidi
Aidha Sven, amesisitiza kuwa hana tatizo lolote na Ajib, adhabu aliyompa ilikuwa kwa ajili ya kumkumbusha umuhimu wa kuzingatia maelekezo anayopewa
"Ajibu amerejea mazoezini na ana shauku kubwa ya kurejesha ubora wake. Hatua tulizochukua juu yake ni katika kumfanya awe mchezaji bora. Kila mchezaji anawajibika kuwa na nidhamu na kufuata yake tunayoelekeza, kama klabu, tumekubaliana hivyo," amesema
Ajibu aliripoti mazoezini jana na moja kwa moja akapewa program yake sambamba na Francis Kahata aliyetua mwishoni mwa wiki