Kiungo Mzambia Clatous Chama anatarajiwa kurejea nchini wakati wowote baada ya taratibu za usafiri kukamilishwa na uongozi wa Simba, imefahamika
Taarifa za ndani ya uongozi wa Simba zimebainisha kuwa hawana wasiwasi na ujio wa Chama kwani kila kitu kwa ajili ya safari yake kimekamilika, changamot bado ipo kwa nyota wawili Francis Kahata na Sharaff Shiboub
Kahata amekwama kwao nchini Kenya, nchi hiyo ikiwa bado imefunga mipaka kutokana na janga la corona
Changamoto kama hiyo pia inamkabili Shiboub ambaye pia inaelezwa uongozi wa Simba unataka kumuongeza mkataba
Luis Miquissone na Meddie Kagere wao wamewasili mapema ambapo jana walishiriki mazoezi ya kwanza yaliyofanyia uwanja wa Mo Simba Arena
Tayari Bodi ya Ligi imetangaza kuwa ligi kuu itarejea Juni 13 wakati droo ya hatua ya robo fainali kombe la FA itafanyika kesho