Rage afafanua sakata lake na TAKUKURU

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 May 2020
Rage afafanua sakata lake na TAKUKURU

Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Simba, Ismael Aden Rage ambaye juzi alishikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) kwa tuhuma za rushwa na kuanza kampeni za uchaguzi mkuu kabla ya wakati kabla ya kupewa dhamana amesema kuwa hakukutwa akitoa hela .

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Tabora, Mussa Chaulo ilisema kuwa mnamo Mei 23, 2020, Rage ambaye ni Mkurugenzi wa Voice of Tabora alishikiliwa baada ya TAKUKURU kupata taarifa kutoka chanzo cha siri kikieleza kuwa Mbunge huyo wa zamani wa Tabora Mjini amedaiwa kuanza kampeni za uchaguzi kabla ya wakati.

Ili kutoharibu uchunguzi unaondelea, Rage aliwekwa mahabusu kuanzia Mei 23 hadi Mei 24 ambapo aliachiwa kwa dhamana.

"Uchunguzi wa taarifa hii unaendelea na mara utakapokamilika taarifa kamili itatolewa kupitia vyombo vya habari," ilieleza taarifa hiyo ya Mkuu wa Takukuru mkoa Tabora, Mussa Chaulo.

Rage amefafanua : "Mimi TAKUKURU hawajanikuta mahala popote natoa hela wala hawajanikuta popote na wanachama wa CCM. Walinifuata nikiwa nafuturu wakaniambia alhaji wewe malizia futari halafu tutazungumza"

GPL

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
6h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
12h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
15h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’