Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa amesema kwa sasa wanaangalia jinsi watakavyorejea katika Ligi Kuu Tanzania Bara na Michuano ya Kombe la Shirikisho (ASFC) na kumaliza kileleni na sio suala la usajili.
Senzo amesema kuwa ligi bado haijaisha, hivyo kwa sasa mawazo yao yote ni kuangalia jinsi watakavyorejea katika Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho na kutwaa ubingwa.
Bingwa wa Ligi Kuu huwakilisha Taifa katika Ligi ya Mabingwa wa Afrika wakati yule wa Kombe la Shirikisho la Azam, hushiriki katika michuano ya Kombe la Shirikisho.
Akizungumzia wachezaji wao wa kimataifa watarejea lini, Mazingiza alisema amekuwa amekuwa akiwasiliana mara kwa mara na mara ya mwisho ilikuwa jana (juzi) na watakaporejea ndio ataujulisha umma.
"Nimekuwa nikiwasiliana na wachezaji wetu walio nje pamoja na makocha na jana tu (juzi) nilizungumza na Meddie Kagere, Francis Kahata , Clatous Chama, Sharaf Shiboub pamoja na makocha na meneja wa timu, " Senzo alinukuliwa na gezeti la Serikali la HabariLeo
Aidha Bosi huyo wa Simba amefafanua kuwa Tanzania ndio imefungua anga lake lakini nchi ambazo wachezaji hao wanatoka mipaka yao haijafunguliwa hivyo hawawezi kusema chochote hivyo kwa vile timu za soka zimeruhusiwa kuanza mazoezi huenda zikawakosa wachezaji wake waliopo nje ya nchi.
Alisema kuwa wachezaji wote wenye mkataba na Simba wataendelea kuwa chini ya klabu hiyo na hawana mpango wowote wa kuwaachia, hivyo kwa sasa hawezi kuzungumzia kuacha au kusajili wachezaji wengine.