Tunafuata njia sahihi kuwa timu kubwa Afrika - Senzo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 May 2020
Tunafuata njia sahihi kuwa timu kubwa Afrika - Senzo

Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba Senzo Mazingisa amesema kwa kiasi kikubwa Simba imepiga hatua na sasa inaweza kuwa kwenye ligi moja na vilabu vikubwa Afrika Kusini kama Orlando Pirates na Kaizer Chiefs

Katika mahojiano na jarida maarufu la Kick-off, Senzo amesema sasa wanafanya jitihada za kuimarisha uchumi wa klabu ili waweze kuwa na ushindani sawa na timu kubwa barani Afrika

"Kwenye suala la umaarufu, Simba ni miongoni mwa klabu kubwa barani Afrika. Kwa sasa tunaongoza kwa uungwaji mkono Tanzania na hata Afrika Mashariki kwa ujumla. Tuko miongoni mwa timu zinazofuatiliwa zaidi kwenye mitandao ya kijamii barani Afrika"

"Upande wa miundombinu nako hatuko mbali. Tuna uwanja wetu wa mazoezi 'Mo Simba Arena' ambao una nyasi bandia na asili, tuna kambi yetu binfasi ambayo inakibidhi viwango vyote vya ubora," alisema Senzo

"Upande wa kikosi tuna wachezaji tisa wa kigeni ambao asilimia kubwa wanazitumikia timu za Mataifa yao. Hii inamaanisha tunashindana kwenye soko la uhamisho na vilabu vikubwa barani Afrika"

"Changamoto kubwa ambayo tayari tumeweka mikakati ni kuimarisha uchumi wetu ili tuweze kuwa na nguvu za kushindana sawasawa na vilabu vingine ambayo vimejiimarisha kiuchumi"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’