Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera anatarajiwa kuwasili usiku wa kuamkia leo kuungana na kikosi cha Yanga kinachokwenda Mwanza kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu na kombe la Shirikisho
Msemaji wa klabu ya Yanga Antonio Nugaz amesema Zahera ataungana na timu siku ya Ijumaa au Jumamosi tayari kwa safari ya mkoani Mwanza wanayotarajia kuifanya Jumapili, Oktoba 20
Yanga inakabiliwa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbao Fc Oktoba 22 ambao utapigwa uwanja wa CCM Kirumba
Zahera alikuwa Congo kutimiza majukumu ya timu ya Taifa
Atakuwa na takribani wiki moja ya kukiandaa kikosi chake kabla ya kuivaa Payramids Fc kwenye mchezo wa kwanza wa play-off kombe la Shirikisho utakaopigwa Oktoba 27 jijini Mwanza
ADVERTISE HERE