Kiungo mshambuliaji wa Simba Hassan Dilunga amefichua kuwa ana shauku ya kupata nafasi ya kucheza soka la kulipwa nje ya nchi
Dilunga ambaye mkataba wake na Simba unamalizika mwishoni mwa msimu, amebainisha kuwa suala la kwenda kucheza nje ya nchi amelipa kipaumbele licha ya kuwa tayari amepewa ofa ya kuongeza mkataba mpya na Simba
Kiungo huyo wa zamani wa timu za Yanga, Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar, amesema amemuachia majukumu Meneja wake kufuatilia mchakato huo
"Kila mtu anafanya kazi avuke pale alipo, anahitaji atoke hapa aende pale na kitu kikubwa ni kumuachia Mungu kila kitu kiende salama"
"Kila mchezaji ana malengo ya kwenda mbali, naimani huu ndio wakati wangu, nishaongea na meneja ili tutoke kidogo, nataka kutoka Tanzania na kwenda kwingine japo siwezi kusema niende huku wala kule ila ikitokea nchi yoyote nitapata nafasi ya kwenda basi sawa, " amesema Dilunga
Dilunga amekuwa na msimu mzuri katika kikosi cha Simba akifunga mabao saba na kutoa pasi tatu za mabao