Bodi ya Shirikisho la mpira wa miguu duniani (IFAB), imeidhinisha mapendekezo ya mabadiliko ya wachezaji watano badala ya watatu wakati ligi zitakaporejea kutokana na janga la corona
Mapendekezo hayo yalitolewa na FIFA wiki iliyopita yakiwa na lengo la kuwasaidia wachezaji kurejea mchezoni salama baada ya kukaa nje kwa muda mrefu ligi zikisimama kuepusha maambukizi ya corona
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limethibitisha kuwa watatumia sheria hiyo pale ligi itakaporejea
Kadau amesema hawana sababu ya kupinga uamuzi huo ambao una lengo zuri kulinda afya za wachezaji na kuzisaidia timu kufanya vizuri
"Uamuzi wa IFAB ni maelekezo hivyo hatuna haja ya kupinga kwani lengo lake ni kulinda afya za wachezaji na hasa kutokana na janga hili la corona," amesema Kidao
FIFA imefafanua kuwa sheria hiyo itatumika wakati huu wa kumaliza misimu ya 2019/20 na huenda ikatumika msimu 2020/21 pia
