Hatma ya Yanga Shirikisho itaamuliwa na washambuliaji - Mziba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Oct 2019
Hatma ya Yanga Shirikisho itaamuliwa na washambuliaji - Mziba

Wakati Yanga ikianzia nyumbani Oktoba 27 kuikabiri Pyramids ya Misri baada ya kushushwa Kombe la Shirikisho, mshambuliaji nyota wa timu hiyo, Abeid Mziba amewapa mchongo washambuliaji wa timu hiyo.

Yanga itacheza na Pyramids nyumbani kabla ya kurudia Novemba 3 mjini Cairo mechi ambayo Yanga inahitaji ushindi ili kujihakikisha kutinga hatua ya makundi kwenye shirikisho.

Mziba amewapa mchongo washambuliaji wa Yanga kuelekea kwenye mechi hiyo akiwasisitiza kuutumia mchezo huo kutengeneza majina yao.

"Pyramids imeshikilia tiketi ya Yanga kimataifa, ni mechi ya kufa na kupona, lakini ndiyo ya kuwatengenezea majina washambuliaji wa timu hiyo.

"Tangu msimu umeanza, binafsi sijaona jambo ambalo wamelifanya la kuibeba timu, hivyo basi wajipange kwa Wamsri waonyeshe kiwango bora, wathibitishe uwezo wao kule," alisema akibainisha kuwa kwenye safu ya ulinzi hakuna tatizo japo nao wanapaswa kuongeza umakini.

Alisema wapinzani hao wa Yanga sio timu nyepesi, timu yake hiyo ya zamani isipofanya maandalizi ya kina isishangae kufungwa nyumbani na ugenini.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’