Vilabu Ligi Kuu valia ukata

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 May 2020
Vilabu Ligi Kuu valia ukata

Athari za changamoto ya ugonjwa wa corona zimeanza kuvitesa vilabu nchini kufuatia kusimama kwa shughuli mbalimbali za michezo kwa zaidi ya siku 50

Baadhi ya timu za Ligi Kuu na zile za Daraja la Kwanza zimetoa malalamiko ya 'ukata' unaowakabili baada ya kusimama kwa ligi kwa karibu miezi miwili sasa kutokana na janga hilo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Stephen Mguto alisema jana kuwa njaa imetawala, kwani karibu timu zote zinalia njaa, Bodi ya Ligi inalia njaa, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linalia njaa.

Mguto akizungumza na Kipindi cha Michezo cha Sports Arena cha Wasafi FM jana, alisema corona ndio chanzo cha hayo yote na wao kama Bodi ya Ligi wanaona imani kwa hilo.

Alisema na wao chanzo chao kikubwa cha fedha ni kama klabu, ambavyo ni viingilio vya milangoni, haki za Televisheni na wadhamini Vodacom, hivyo hawana wigo mpana wa mapato, na sasa hawapati kitu baada ya ligi kusimama.

Alikiri kuwa na wao Bodi ya Ligi wanalia njaa kutokana na hali ilivyo sasa na kikubwa cha kulaumiwa ni corona, na kama isingekuwepo, basi kilio hicho kisingekuwa kikubwa kama sasa.

Alisema sekretarieti yao inatarajia kukutana na wadhamini ili kuzungumzia suala hilo, kwani hata ligi itakapoendelea itachezwa bila mashabiki, hivyo klabu bado zitaendelea kukabiliana na njaa, kwani hawatakuwa na kipato.

Alisema wana mengi ya kuangalia jinsi ya kupunguza makali hayo kwa timu, hivyo watakaa na wadhamini kuona wanafanya nini.

TFF juzi ilikaririwa ikisema kuwa kuruhusu mashindanio yake yote kuendelea itategemea uamuzi wa serikali, ambayo itaelekeza muda muafaka wa kurejea kwa mashindano.

Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo alikaririwa na gazeti la HabariLeo jana akisema kuwa shirikisho hilo bado linaendelea na mchakato wa ndani kwa kushirikiana na Bodi ya Ligi (TPLB) kuelekea kurejea kwa Ligi Kuu Tanzania Bara.

"TFF kuhakikisha ligi zinarejea, itategemea tamko la serikali juu ya mwenendo wa janga la virusi vya corona, hivyo wanachama wanapaswa kutekeleza agizo la awali la kuepuka mikusanyiko, "alisema Ndimbo.

Tayari Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almasi Kasongo alisema hivi karibuni kuwa Ligi Kuu itaendelea mwanzoni mwa mwezi ujao na haitakuwa na mashabiki, huku wachezaji, waamuzi, viongozi na waandishi wa habari kupimwa corona kabla ya kuingia uwanjani.

Hivi karibuni Rais John Pombe Magufuli wakati akimuapisha Waziri wa Sheria na Katiba, Dk Mwigulu Mchemba alisema kuwa anawasiliana na washauri wake kuangalia ligi iendelee lini nchini.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’