Simba yajipanga kuwarudisha 'Maproo' wake

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4 May 2020
Simba yajipanga kuwarudisha 'Maproo' wake

Baada ya Bodi ya Ligi kubainisha kuwa tayari imepeleka mapendekezo kwa Serikali kuhusu utaratibu watakaotumia kumalizia mechi zilizobaki ligi kuu ya Vodacom, uongozi wa Simba unajipanga kuwarudisha wachezaji wake wa kigeni ambao wako nje ya nchi

Ligi Kuu huenda ikaanza kutimua vumbi mwezi Juni kumaliza raundi 10 zilizosalia baada ya Rais wa nchi Dk John Magufuli kubainisha kuwa anafikiria kutoa ruhusa ligi hiyo iendelee

Baadhi ya wachezaji wa kigeni ambao waliitwa kujiunga na timu za Taifa mwezi wa tatu, walishindwa kurejea nchini baada ya nchi zao kufunga mipaka huku nyingine zikisitisha safari za ndege za Kimataifa kutokana na janga la corona

Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa amesema wanafikiria utaratibu wa kuweza kuwarudisha wachezaji hao mapema ili waweze kuungana na wenzao ambao wako nchini

"Tunasubiri ni lini timu zitaruhusiwa kuanza mazoezi lakini tunaangalia namna ambavyo tunaweza kufanya mchakato wa kuwarudisha wachezaji wetu ambao wako nje ya nchi tangu mechi za timu za Taifa zilipofutwa," amesema Senzo

Miongoni mwa wachezaji ambao wako nje ya nchi ni mshambuliaji Meddie Kagere, kinara wa mabao kwenye ligi kuu ya Vodacom akiwa ametupia kambani mabao 19

Wengine ni Clatous Chama, Francis Kahata, Sharaff Shiboub na Luis Miquissone aliyejiunga na Simba mwezi Januari

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
19h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’