Zahera atamba, Yanga iko tayari kucheza na yeyote Shirikisho

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Oct 2019
Zahera atamba, Yanga iko tayari kucheza na yeyote Shirikisho

Wakati droo ya hatua ya mtoani kombe la Shirikisho ikitarajiwa kufanyika leo nchini Misri, kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema timu yake iko tayari kucheza na timu yoyote watakayo pangwa nayo

Zahera aliyerejea Congo kutimiza majukumu ya timu ya Taifa, amesema soka la Afrika limebadilika kulinganisha na miaka ya nyuma kwa kuwa viwango vya wachezaji vinafanana

Amesema baada ya kutolewa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa, hesabu zake ni kuhakikisha wanatinga makundi kombe la Shirikisho

Zahera amesema amejifunza mambo mengi kutokana na kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, na kwamba atarekebisha makosa waliyoyafanya ili yasijitokeze Kombe la Shirikisho

Timu za waarabu hasa Misri zimekuwa zikiipa changamoto Yanga kwenye michuano ya Kimataifa

Pyramids Fc ya Misri na Paradou AC ya Algeria ni miongoni mwa timu zinazoweza kupangwa na Yanga leo

Nyingine ni ESAE ya Benin, DC Motema Pembe (DRC), FC San Pedro (Ivory Coast), Bandari (Kenya), Bidvest Wits (Afrika Kusini), TS Galaxy (Afrika Kusini), Proline (Uganda) ama Triangle United ya Zimbabwe.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
11h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
15h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
20h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
23h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’