Kutokana na janga la corona kuendelea kuwa changamoto ya dunia, mashirikisho ya soka nchi mbalimbali yamechukua hatua za kumaliza misimu yao ya soka
Majirani zetu Kenya wamekuwa nchi ya kwanza ukanda wa Afrika Mashariki kumaliza msimu wao huku wakiitangaza Gor Mahia kuwa mabingwa
Shirikisho la soka Kenya (FKF) limetumia msimamo wa ligi wa duru ya kwanza kufikia maamuzi hayo kulingana na katiba ya Shirikisho hilo
Hapa Tanzania mjadala wa nini kifanyike kutokana na corona kuendelea kuwa changamoto, umeshika kasi
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linasubiri mwongozo wa Serikali kabla ya kutangaza msimamo wake
Lakini ni wazi vinara wa ligi kuu Simba wanaweza kutetea ubingwa wao kwa msimu wa tatu mfululizo
Iwe kwa mechi zilizobaki kuchezwa au kwa kutumia msimamo wa duru ya kwanza au wa sasa
Ifahamike Tanzania itahitaji wawakilishi wa michuano ya CAF kwa ajili ya msimu ujao
Hivyo kama ligi itafutwa lazima TFF ije na mwongozo wa kutoa wawakilishi kwa ajili ya michuano hiyo
Simba kama bingwa mtetezi,a ana kila sababu ya kuiwakilisha nchi kwenye michuano hiyo msimu ujao