Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema licha ya mapungufu yanayokikabili kikosi cha timu hiyo, ameridhishwa na kiwango kinachoonyeshwa na wachezaji
Dk Msolla jana alikuwepo uwanjani kuwashuhudia vijana wake wakipepetana na Coastal Union katika mchezo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa bao moja kwa bila
Akizungumza baada ya mchezo huo, Dk Msolla ambaye kitaaluma ni kocha, ameeleza kuridhishwa na alichokiona
"Timu imecheza vizuri ingawa naona bado kuna mapungufu kwenye umaliziaji," alisema Dk Msolla
"Nimeridhishwa kuona wachezaji wameanza kuzoeana kwani timu inaonekana kucheza kwa mipango"
"Changamoto inayotukabili sasa niliitarajia kwa kuwa hatukuwa na maandalizi ya kutosha kabla ya kuanza msimu kutokana na muingiliano wa ratiba"
"Kulikuwa na michuano ya Afcon lakini pia ligi ya mabingwa ilianza mapema tofauti na misimu mingine. Wachezaji walianza msimu kwa kucheza mechi ngumu"
"Wametumia nguvu nyingi kwenye michuano hiyo huku wakikosa muda wa kutosha kukaa sawa"
DK Msolla amewaomba wanachama kuwa wamoja timu inapokuwa na matokeo mabaya, kwani haina maana kuanza kulaumiana kwa sababu jambo hilo
haliwezi kujenga timu.