Mabingwa wa nchi Simba wanatarajiwa kuiongezea nguvu safu yao ya ulinzi katika dirisha la usajili ambalo litafunguliwa baada ya msimu huu kumalizika
Taarifa za ndani zimebainisha kuwa Simba imevutiwa na mlinzi wa KCB ya Kenya Mike Kibwage
Beki huyo mwenye umri wa miaka 23, amekuwa na msimu mzuri kwenye ligi kuu ya Kenya ambayo imesimama kama ilivyokuwa hapa Tanzania kutokana na janga la corona
Mmoja wa maafisa wa timu hiyo amefichua kuwa ingawa bado hawajapokea ofa rasmi kutoka klabu ya Simba kwa ajili ya mchezaji wao, lakini Simba iliulizia kuhusu mkataba wake
"Tunafahamu Simba wamevutiwa na mchezaji wetu, kama wataleta ofa basi itajadiliwa lakini muhimu tutafanya maamuzi ambayo yatakuwa ya faida kwa mchezaji," alisema bosi huyo wa KCB
Aidha kwa upande wa Kibwage amesema yeye kama mchezaji yuko tayari kujiunga na timu yoyote ambayo itafikia nae makubaliano
Amesema bado hajapokea ofa rasmi kutoka klabu ya Simba