Bado mechi 36, mapambano yanaendelea

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Oct 2019
Bado mechi 36, mapambano yanaendelea

Baada ya kuanza msimu kwa kufungwa na jana kulazimishwa sare ya mabao 3-3, matokeo hayo hayawafurahishi mashabiki wa klabu ya Yanga

Ni matokeo yaliyowaumiza Wanayanga ambao bado wanasubiri furaha ya kudumu kutoka kwa timu yao

Hata hivyo bado ni mapema sana kukata tamaa kwani pamoja na kutopata ushindi, kiwango cha timu kimeendelea kuimarika

Yanga bado ina michezo 36 ya kuwania ubingwa

Kuanza na mwanzo mbaya sio tatizo, muhimu ni kujipanga kuhakikisha timu haiendelei kufanya makosa.

Nakumbuka msimu uliopita hata Simba iliyotwaa ubingwa ilianza hivi

Katika mechi zao tatu za mwanzo, walishinda mechi moja tu dhidi ya Prisons

Walitoka sare na Ndanda Fc na baadae kuchapwa na Mbao bao 1-0

Keshokutwa Yanga inarejea uwanja wa Uhuru kuikabili Coastal Union

Mchezo huo unawapa wachezaji nafasi ya kurejesha furaha ya mashabiki kwa kuibuka na ushindi

Kwani ili Wanayanga waendelee kuiunga mkono timu, wanahitaji furaha

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’