Kiungo wa Simba Francis Kahata ni miongoni mwa wachezaji ambao wamekwama kurejea nchini kutokana na janga la corona
Kahata yuko kwao Kenya alikokuwa amekwenda kwa ajili ya masuala binafsi lakini ameshindwa kurejea baada ya nchi hiyo kuzuia safari za Kimataifa
Corona imepelekea nchi nyingi ikiwemo Tanzania kuchukua hatua kama hiyo katika jitihada za kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo
Nyota wengine wa Simba ambao wako nje ya nchi ni Clatous Chama, Sharaff Shiboub, Luis Miquissone na Meddie Kagere hawa walirejea makwao baada ya kuitwa katika timu za Taifa
Kahata amesema Kenya kuna marufuku ya kutotoka nje kwa muda wa siku 21 hivyo analazimika kufanya mazoezi nyumbani kwake
Amesema kutokana na kasi ya maambukizi ya ugonjwa wa corona nchini Kenya wanapaswa kuchukua tahadhari zaidi ambapo wakati mwingine amelazimika kufanya mazoezi akiwa na barakoa
Kiungo huyo fundi amesema anasubiri maelekezo kutoka mamlaka husika ili aweze kurejea nchini kuendelea na majukumu yake kunako klabu ya Simba