Corona imechelewesha mkataba wa Kagere - Gakumba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
25 Apr 2020
Corona imechelewesha mkataba wa Kagere - Gakumba

Licha ya kuhusishwa na timu nyingi kutaka kumsajili kinara wa mabao Ligi Kuu Bara, Mnyarwanda Meddie Kagere, ambaye mkataba wake na Simba unaelezwa kumalizika msimu huu, wakala wa mshambuliaji huyo, Patrick Gakumba amewatuliza mashabiki wa timu hiyo baada ya kueleza kuwa tayari mazungumzo na Simba ili kumuongeza mkataba mpya yamekamilika

Mshindi huyo wa kiatu cha dhahabu Ligi Kuu Bara msimu uliopita, hadi ligi hiyo inasimama msimu huu yupo kileleni mwa orodha ya wafungaji akiwa na mabao 19 wakati huu Simba ikiwa imebakiza mechi 10 kabla ya ligi kumalizika

Gakumba amesema Kagere ataendelea kubaki Msimbazi, kinachosubiriwa ni kuja kusaini mkataba mpya

"Ni kweli mkataba wa Kagere unamalizika, lakini tumeshafanya mazungumzo na kukubaliana na kilichobaki ni kuja kuchukua mamilioni kutoka kwa Mo, kinachotuzuia ni kutokana na mipaka ya nchi kufungwa baada ya kuibuka mlipuko wa virusi vya corona," alisema.

Gakumba alisema Mo hawezi kushindwa kumbakisha mchezaji huyo anayeongoza kwa mabao Ligi Kuu na kwamba kila kitu wameshakubaliana.

Awali kulikuwa na tetesi kuwa klabu ya APR ilikuwa ikimuwania kinara huyo wa mabao lakini jana uongozi wa APR ulikanusha

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’