Mabingwa wa kihistoria Tanzania Yanga leo wanarejea kwenye mikikimikiki ya ligi kuu wakiwa wenyeji wa Polisi Tanzania katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Uhuru
Wakati ligi hiyo ikiwa imeingia raundi ya tano, Yanga imeshuka dimbani mara moja na leo utakuwa mchezo wa pili kutokana na ushiriki wake kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa
Ni mchezo ambao Yanga inahitaji kuondoka na alama zote tatu hasa ikizingatiwa ilipoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Ruvu Shooting
Matokeo tofauti na ushindi huenda yakaongeza presha kwa benchi la ufundi la timu hiyo linaloongozwa na kocha Mwinyi Zahera
Hata hivyo Mcongomani huyo leo atawashuhudia vijana wake akiwa jukwaani akianza kutumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu
Mchezo utapigwa saa kumi jioni kiingilio ni Tsh 15,000/- VIP na Tsh 5,000/- mzunguuko