Kagere mmoja ni sawa na washambuliaji wanne Yanga..!

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
20 Apr 2020
Kagere mmoja ni sawa na washambuliaji wanne Yanga..!

Mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere mpaka ligi Kuu Tanzania Bara inasimama kutokana na janga la virus vya Corona, alikuwa amefunga mabao 19.

Idadi hiyo ya mabao ambayo Kagere amefunga, ni sawa na mabao ya wachezaji wanne katika kikosi cha watani zao Yanga

Katika kikosi cha Yanga, anayeongoza kwa ufungaji ni David Molinga raia wa DRC mwenye mabao nane, akifuatiwa na Patrick Sibomana kutoka Rwanda mwenye matano.

Wengine ni Bernard Morrison raia wa Ghana ameziona nyavu za wapinzania mara tatu, akiwa sawa na Mtanzania Tariq Seif.

Nyota hao wanne wa Yanga jumla wamefunga mabao 19 ambayo ni sawa na yale yaliyowekwa kambani na Kagere peke yake.

Kagere yuko kwenye nafasi nzuri ya kutwaa kiatu cha dhahabu katika msimu wa pili mfululizo

Katika msimu wake wa kwanza kwenye Ligi Kuu Bara, Kagere aliweza kuwa mfungaji bora baada ya kufunga mabao 23 na hivyo kuchangia Simba kutwaa ubingwa wa ligi hiyo 2018/19.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
25m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
3h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
21h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’