Gakumba afichua dili la Kagere na Levante

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Apr 2020
Gakumba afichua dili la Kagere na Levante

Wakala wa mshambuliaji hatari wa Simba Meddie Kagere amefichua kuwa klabu ya Levante inayoshiriki ligi kuu ya Hispania 'La Liga' imevutiwa na uwezo wa mtupia mabao huyo hatari ligi kuu ya Vodacom

Katika mahojiano na kipindi cha michezo cha Radio One, Patrick Gakumba amesema Levante imemuulizia Kagere ambaye wamedai kumuona kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Sevilla

Hata hivyo Gakumba amesema wamelipotezea dili hilo baada ya kutoridhishwa na masharti yake. Amesema anasubiri kumalizana na Simba ili Kagere asaini mkataba mpya kuendelea kukipiga Msimbazi

"Levante wameniambia Meddie Kagere wamemfatilia na kumuona kwenye mechi ya Simba na Sevilla na wamemfuatilia akiwa Rwanda na Kenya akiwa mfungaji bora lakini tumeshindwana kidogo tu"

"Kwa sababu wao wanachotaka ni kwamba aende pale acheze mechi za majaribio lakini Meddie kagere sio wakucheza mechi za majaribio na pesa walizoniambia wanasema wanataka kwanza wamuangalie Muda wa miezi sita"

"Kagere sio mchezaji wa majaribio niliisha waambia nyinyi yule atacheza mpaka wale wanaomuita mzee watachoka. Walianza kumuita mzee miaka mitano iliyopita na kila wanapomwambia anafunga na mimi ninachoangalia ni magoli na siangalii umri,"alisema Gakumba

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
4h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’