Sven amtaja Kikoti wa Namungo Fc

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14 Apr 2020
Sven amtaja Kikoti wa Namungo Fc

Wiki iliyopita Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, alimtaja mchezaji anayemkosha katika Ligi Kuu Tanzania ambaye si mwingine bali ni kiungo wa Namungo FC, Lucas Kikoti.

Sven alimtaja mchezaji huyo, Jumamosi iliyopita wakati alipokuwa akijibu maswali ya mashabiki wa soka kupitia mitandao ya kijamii ya Simba.

Kati ya maswali aliyoulizwa ni kumtaja mchezaji aliyemvutia kutoka timu alizocheza nazo tangu ametua katika ardhi ya Tanzania ambapo bila kusita, alimtaja Kikoti.

Sven alisema mchezaji huyo alimwangalia vizuri katika mechi waliyokutana na Namungo ambayo Simba iliibuka na ushindi wa mbao 3-2 kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Alisema katika kumwangalia nyota huyo, alibaini ni kati ya wachezaji waliojaaliwa kipaji cha hali ya juu, akitolea mfano bao alilowafunga kuwa lilidhihirisha ubora na umakini wake.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
48m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’