Tshabalala anasubiri kucheza fainali ligi ya mabingwa Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
13 Apr 2020
Tshabalala anasubiri kucheza fainali ligi ya mabingwa Simba

Nahodha Msaidizi wa Simba Mohammed Hussein 'Tshabalala' amesema jambo analolifikiria zaidi ni kuiona klabu yake ikicheza fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Tshabalala alikuwa sehemu ya kikosi kilichofanya mambo makubwa mwaka juzi baada ya kufanikiwa kutinga robo fainali ya michuano hiyo wakitolewa na TP Mazembe kwa kufungwa mabao 4-1 baada ya matokeo ya suluhu ya bila kufungana kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam

Tshabalala amesema baada ya mafanikio waliyopata mwaka juzi, kila mchezaji ana kiu ya kuona wanafika fainali ya michuano hiyo mikubwa kabisa barani Afrika kwa ngazi ya vilabu

"Kila mchezaji hapa kwetu anahitaji kuona mafanikio, kubwa ni kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa, hali hiyo inatulazimu tupambane kuhakikisha tunachukuwa ubingwa na kujipanga kwa michuano hiyo ya kimataifa," amesema Tshabalala.

Beki huyo mahiri kwa upande wa kushoto kwa Tanzania sasa,  amesema anashirikiana na wenzake katika kufikia malengo yao hayo akiamini kujituma kwao kutawezesha kuwapa mashabiki kile wanachokitarajia.

"Kwa kipindi hichi cha mlipuko wa virusi vya corona, tupo makini sana kwa sasa, nafanya mazoezi binafsi kwa kufuata maelekezo ya benchi la ufundi huku nikijilinda na kuzingatia yale yaliyokatazwa na wizara ya afya"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
13h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
19h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
22h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’