Achana na zile tetesi zilizokuwa zikiihusisha klabu ya Simba na kiungo wa Yanga Papy Tshishimbi kwani Mtendaji Mkuu wa mabingwa hao wa nchi Senzo Mazingisa alikanusha kuwa hawakuwahi kumuhitaji Mcongomani huyo
Lakini habari zilizotoka jikoni inaelezwa ni kweli Simba ina mpango wa kusajili kiungo mkabaji, ambapo jina la nyota anayekipiga AS Vita Jeremy Mumbere limetajwa
Mumbere ni mmoja wa wachezaji wanaofanya vizuri kwenye kikosi cha timu hiyo
Mcongomani huyo anatajwa kuja kuongeza nguvu kwenye safu ya kiungo cha ukabaji ambacho kimekuwa kikimtegemea zaidi Jonas Mkude na Gerson Fraga raia wa Brazil
Ni katika mkakati wa kutengeneza kikosi imara ambacho kitafanya vizuri kwenye michuano ya ligi ya mabingwa baadae mwaka huu
ADVERTISE HERE