Maandalizi ya mchezo baina ya Taifa Stars dhidi ya Sudan yamekamilika ambapo Shirikisho la soka nchini (TFF), limewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani kuishangilia timu ya taifa
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari mapema leo, Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao alisema shirikisho limejipanga vyema kuhakikisha Stars inapata ushindi kwenye nchezo huo utakaopigwa uwanja wa Taifa, Jumapili Septemba 22 saa moja jioni
"TFF kwa maana ya kiutendaji tumejipanga vizuri kwa ajili ya mechi hiyo. Timu tumeiweka kwenye kambi yenye hadhi ya juu katika Hoteli ya nyota tano ya Hyatt Hotel na wachezaji wote wako kwenye hali nzuri," alisema
"Masuala mengine yote kwa maana ya posho na yale ambayo tunahitajika kufanya tumeshayatimiza hivyo kilichobaki ni mchezo wenyewe.
"Kikubwa tunawaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuipa hamasa na sapoti timu. Na ni jambo jema kama watawahi mapema kabla ya kuanza kwa zoezi la kupasha misuli, muda ambao kisaikolojia mchezaji utayari wa mechi kwa mchezaji unaanza"
Kiingilio cha mcheo huo ni Tsh 2,000/- tu
Stars inahitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga fainali za michuano ya CHAN kwa wachezaji wanaocheza ndani ambazo zitafanyika mwakani nchini Cameroon
Mchezo wa marudiano baina ya timu hizo utapigwa Oktoba 18 nchini Uganda