Ni heshima kubwa kucheza Simba - Tshabalala

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
8 Apr 2020
Ni heshima kubwa kucheza Simba - Tshabalala

Mlinzi wa kutumainiwa ndani ya kikosi cha Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ amesema anajivunia kuwa miongoni mwa wachezaji ndani ya kikosi bora cha Simba.

Tshabalala miongoni mwa nyota wenye nidhamu ya hali ya juu ndani na nje ya uwanja ana uhakika wa namba ndani ya kikosi chake licha ya kuwa na ushindani dhidi ya mkali mwenzie, Gadiel Michael, aliyetua kutoka kwa mahasimu, Yanga.

Nahodha huyo msaidizi amesema anajisikia faraja kuwa sehemu ya kikosi cha mabingwa hao wa Tanzania Bara

"Nafurahi kuwa hapa na pia kwangu mimi ni heshima kubwa kuchezea Simba, nitazidi kupambana kuhakikisha nakilinda kiwango changu ili nizidi kupata namba chini ya kocha yoyote atakayeinoa Simba," amesema

Aidha Tshabalala anasema, katika kumbukumbu za maisha yake katika soka, hatasahau kuwa alikuwa sehemu ya wachezaji walioipeleka Simba hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

"Hili jambo halitafutika maishani mwangu, ni historia na itakuwa kumbukumbu yangu maishani"

Nyota huyo amesisitiza mafanikio ambayo klabu yake inayapata yanatokana na umoja uliopo ndani ya timu yao kuanzia viongozi, wachezaji mpaka mashabiki wao.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
11h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’