Mabosi Simba kukutana leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
31 Mar 2020
Mabosi Simba kukutana leo

Vigogo wa klabu ya Simba wanatarajiwa kukutana leo kujadili mikakati mizito na kuwekana sawa mipango ya klabu hiyo kuelekea msimu wa 2020/21

Kikao hicho kitahusu mikakati ya mechi zilizosalia, usajili mpya na hatma ya mastaa wao walioko nje ya nchi kwani hata katika kikao cha leo walipaswa kuwepo

Awali uongozi ulipanga wachezaji wote wawepo kwenye kikao cha leo lakini kutokana na baadhi yao kushindwa kuripoti Dar kwa wakati wameamua viongozi wakutane wenyewe kwanza halafu wawape muongozo wachezaj

Tayari siku saba ambazo waliwapa mapumziko wachezaji mapumziko zimemalizika na leo watakubaliana muongozo mpya ili kuhakikisha hawapotezi uelekeo wa ubingwa na mikakati yao

Kwa upande wa mikakati ya kambi, wachezaji walio nje ya nchi Meddie Kagere (Rwanda), Luis Miquissone (Msumbuji), Francis Kahata (Kenya) na Clatous Chama (Zambia) wapo makwao ambapo baadhi watashindwa kurejea kwa wakati kutokana na serikali za nchi yao kuzuia safari za nje

Endapo baadhi watafanikiwa kuingia nchini basi watalazimika kuwa chini ya uangalizi kwa siku 14 jambo ambalo Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa amesema wanakubalina na agizo la serikali kwamba mtu yoyote atakayeingia nchini lazima akae karantini

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’