Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli jana alibainisha kuwa wageni wote wanaoingia Tanzania kutoka nje ya nchi watalazimika kubaki kwenye uangalizi kwa siku 14 kabla ya kuruhusiwa kuchanganyika na watu wengine
Ni katika jitihada ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona ambapo mpaka sasa watu 12 wamethibitika kuambukizwa nchini
Agizo hilo la Rais linaondoa utata uliowekwa na TFF juu ya nyota wa kigeni waliosafiri makwao kuwa wangezuiwa kurudi nchini na pengine hata kuzuiwa kushiriki ligi kuu
Hii ina maana mshambuliaji Meddie Kagere na kiungo Clatous Chama ambao waliruhusiwa kusafiri kwenda kuona familia zao, wakirejea watakuwa kwenye uangalizi wa siku 14 kabla ya kuendelea na majukumuu yao
ADVERTISE HERE