Baada ya Afisa habari wa Simba Haji Manara kuwataka wapenzi, wanachama na mashabiki wa Simba kukaa kimya kuelekea mchezo dhidi ya Yanga, klabu hiyo imeingia hofu kuwa itakosa mapato kutoka kwa mashabiki wa Simba
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amelalamikia uamuzi huo wa Wana Msimbazi kukaa kimya akihofia kuwa mashabiki wengi hawatajitokeza uwanjani
Lakini pengine ni kutokana na ukweli kuwa klabu ya Simba ndio yenye uwezo wa kujaza uwanja wa Taifa hivyo uamuzi wa kukaa kimya unaweza kuwapunguzia mapato
Viongozi hao wa Yanga wameshauriwa kutangaza mechi hiyo kwani mchezo huo wa pili ni wa kwao kwa kuwa wao ni wenyeji
Mashabiki wengi waliingia kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Januari 04 kutokana na juhudi kubwa zilizofanywa na viongozi wa klabu ya Simba wakiongozwa na Haji Manara ambaye ndiye Afisa Habari na mwamba wa masuala ya promo