Jioni hii kikosi cha Yanga kitakuwa kwenye uwanja wa Taifa wa Botswana kufanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers kesho
Uwanja huo wa nyasi bandia, ukubwa wake unakaribiana na uwanja wa Mkapa
Ili kuhakikisha wachezaji hawatatizwi na 'pitch' ya uwanja huo, uongozi wa Yanga ulitafuta uwanja wa nyasi bandia ambao ndio waliotumia tangu walipowasili Jumanne iliyopita
Township Rollers hawakupenda mchezo wa kesho kupigwa kwenye dimba hilo lakini maombi yao ya kubadili uwanja yalikataliwa na CAF
Kesho Yanga itarejea katika uwanja huo ambao mwaka jana walifanikiwa kupata matokeo ya suluhu ya bila kufungana
Hakuna shaka mambo yatakuwa mazuri kwa upande wa Yanga mwaka huu, kwani nafasi ya kuibuka na ushindi ni kubwa