Karia ateuliwa kusimamia CHAN

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 Jan 2018
Karia ateuliwa kusimamia CHAN
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Ndugu Wallace Karia ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF kuwa kamishna wa mechi ya kwanza ya ufunguzi wa Fainali za Africa kwa wachezaji wa ndani CHAN kati ya Morocco na Mauritania itakayochezwa Januari 13, 2018.

Mchezo huo ambao Rais Karia atausimamia akiwa Kamishna utachezwa kwenye Uwanja wa nyasi asilia wa Mohamed V huko Casablanca.

Waamuzi watakaochezesha mchezo huo ni Janny Sikazwe kutoka Zambia atakuwa mwamuzi wa katikati akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja kutoka Kenya Marwa Aden Range na mwamuzi msaidizi namba mbili akitokea Msumbiji Arsenio Chandreque Maringula wakati muamuzi wa mezani Louis Hakizimana akitokea Rwanda.

Mchezo huo unaohusisha timu mwenyeji unatarajiwa kufuatiliwa na mashabiki wengi zaidi.

Rais Karia hivi karibuni pia aliteuliwa na CAF kuwa mmoja wa wajumbe wa kamati ya maandalizi ya michuano hiyo ya CHAN itakayoanza Januari 13 mpaka Februari 4, 2018.

Mashindano hayo yanayofanyika kwa mara ya tano (5) bingwa mtetezi akiwa DR Congo.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
13h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
19h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
22h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’