Tutakomaa mpaka mwishoni mwa msimu - Bocco

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14 Feb 2020
Tutakomaa mpaka mwishoni mwa msimu - Bocco

Pamoja na Simba SC kuongoza kwa pointi 53, haimfanyi nahodha wa timu hiyo John Bocco avimbe kichwa badala yake anaona wana kazi ngumu ya kulinda nafasi waliopo.

Bocco amesema kila timu inatamani kukaa kileleni na kwamba bado wana mechi 17 mkononi ambazo wanatakiwa kupambana kwa nguvu zote ili waweze kutetea ubingwa.

Amesema anaamini katika mshikamano kuanzia kwa wachezaji, mashabiki, viongozi na benchi la ufundi kwamba ndio silaha yakuwafanya watwae ubingwa.

"Ukisikia ubingwa maana yake kuna ushindani, anayefanya vyema ndiye anakuwa mbabe kuliko mwingine kwa sasa bado mechi zipo nyingi hivyo vita inaendelea"

"Kila timu kwa sasa inaangalia Simba kuwa kileleni, hilo litafanya waibue ushindani mkali dhidi yetu, ndio maana nasema lazima tuongeze bidii ya kufikia malengo yetu,"amesema.

Mpaka sasa Bocco amefunga bao moja, kutokana na kukaa nje kwa muda mrefu akisumbuliwa na majeraha, amezungumzia hilo kwamba amerejea atapambana.

"Nilitamani kufanya makubwa, unajua Mungu ndiye anajua siri za maisha yetu, sikujua kama ningeumia, kubwa ninaloshukuru nimepona nitaendelea na majukumu yangu,"amesema Bocco

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’