Mlinda lango wa Yanga Ramadhani Kabwili amesema wamejiandaa vyema kuelekea mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers ambao utapigwa kesho Jumamosi saa 12 jioni kwenye uwanja wa Taifa
Akiwakilisha wachezaji wa Yanga kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari, Kabwili amesema wako tayari kwa mchezo huo
"Tumefanya maandalizi mazuri kuelekea mchezo wetu wa kwanza katika mashindano ya klabu bingwa Afrika"
"Tuna matumaini makubwa ya kupata ushindi, tunawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kutuunga mkono"
"Tunahitaji kushinda mchezo wa hapa nyumbani ili tuwe na kazi rahisi ya kukamilisha ratiba kwenye mchezo wa marudiano"
Kabwili ndiye aliyedaka mchezo wa kwanza timu hizo zilipokutana uwanja wa Taifa mwaka jana na Rollers kuibuka na ushindi wa mabao 2-1
Katika hatua nyingine, kocha Msaidizi wa Yanga Noel Mwandila amesema wamekuwa wakijiandaa na mchezo huo kwa takribani wiki nne, hivyo wako tayari
"Tumekuwa tukijiandaa kwa takribani wiki nne. Maandalizi yetu ya mwisho yalikuwa mchezo wa kirafiki jana," amesema
"Tuko tayari kuikabili Township Rollers kesho"