Idadi ya nyota wa kigeni wanaosajiliwa na timu za ligi kuu huenda ikapungua msimu ujao na kuwa watano
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe, amesema timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao zinatakiwa kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi watano
Kauli hiyo ya Serikali imekuja kufunga mjadala wa idadi ya wachezaji wa kigeni wanaopaswa kusajiliwa na vilabu wakati huu TFF ikiruhusu kusajili mpaka wachezaji 10
Kumekuwa na maoni kuwa wingi wa wachezaji wa kigeni unanyima fursa kwa wachezaji wazawa kupata nafasi ya kucheza na pengine kuathiri kiwango cha timu ya Taifa
ADVERTISE HERE