Nyota watatu Yanga hatihati kuikosa Rollers

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Aug 2019
Nyota watatu Yanga hatihati kuikosa Rollers

Wakati kikosi cha Yanga kikitarajiwa kurejea mchana wa leo Ijumaa kutoka visiwani Zanzibar, uongozi wa timu hiyo bado haujapokea leseni za wachezaji watatu kutoka Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF)

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Dismas Ten amesema leseni za Farouq Shikalo, David Molinga na Mustafa Suleyman bado hazijafika

Ten amesema wanafanya mawasiliano na TFF/CAF na wana matumaini ya kupokea leseni za nyota hao kwa wakati ili waweze kuwatumia kwenye mchezo huo

Kuhusu maandalizi ya timu, Ten amesema kikosi chao kimejiandaa vizuri na wana uhakika watawapa furaha mashabiki uwanja wa Taifa kesho

Hivyo amewataka mashabiki wajitokeze kwa wingi kuipa nguvu timu yao

Kikosi cha Yanga kinarejea jijini Dar es salaam leo kikitokea Zanzibar ambako kiliweka kambi ya siku tatu

Ikiwa Zanzibar Yanga ilicheza michezo miwili ya kirafiki, ambapo juzi iliichapa Mlandege Fc mabao 4-1 kabla ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Malindi Fc jana

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
10h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
14h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
15h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
15h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’