FT : Mtibwa Sugar 0-3 Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
11 Feb 2020
FT : Mtibwa Sugar 0-3 Simba

Mabingwa wa nchi Simba leo wametoa onyo kali kwa timu nyingine zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom baada ya kuifumua Mtibwa Sugar mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Jamhuri

Mchezo huo uliohudhuriwa na mamia ya mashabiki wa soka wa mkoani Morogoro na maeneo ya jirani, uliishuhudia Simba ikicheza kandanda safi huku wakiwa bora zaidi mbele ya lango la Mtibwa Sugar

Kalamu ya mabao kwa upande wa Simba ilianza kwenye dakika ya 45 ya mchezo, nahodha John Bocco akiitanguliza Simba kwa bao safi baada ya kupokea pasi ya Meddie Kagere ambaye hilo ni bao lake la sita kutengeneza

Dakika mbili baada ya kuanza kipindi cha pili, Mohammed Hussein aliifungia Simba bao safi la kideoni akifunga akitokea pembezoni mwa lango la Mtibwa

Simba iliendelea kulishambulia lango la Mtibwa Sugar kama nyuki na Hassan Dilunga akaweka kambani bao la tatu kwenye dakika ya 59 akimalizia pasi murua ya Clatous Chama

Ulikuwa mchezo ambao Simba ilidhihirisha kuwa bado inao ubora wake, pengine suala la uchovu linaweza kuwa lilichangia kucheza chini ya kiwango katika michezo iliyopita

Mlinda lango Aishi Manula leo alirejea kikosini na hakika alidhihirisha bado anastahili kuwa kipa namba moja wa Simba

Baada ya mchezo huo Simba itaelekea mkoani Iringa kuifuata Lipuli Fc

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
6h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
12h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
15h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’