Yanga imeichapa Mlandege Fc mabao 4-1 kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa dimba la Amaan leo Jumatano usiku
Kocha Mwinyi Zahera alitumia vikosi viwili tofauti katika kila la kipindi cha mchezo huo wa kujipima

Mabao matatu yalipatikana kwenye kipindi cha kwanza yakifungwa na Juma Balinya, Patrick Sibomana na Sadney Urikhob
Kikosi kilichocheza kipindi cha kwanza ni kilekile kilicholazimishwa sare ya bao 1-1 na Kariobangi Sharks Jumapili
Mrisho Ngasa aliiongezea Yanga bao la nne kwenye kipindi cha pili
Mlandege Fc ilipata bao la kufutia machozi wakati mchezo huo ukielekea ukiongoni
Kesho Alhamisi Yanga itashuka tena dimbani kumenyana na Malindi FC
ADVERTISE HERE