Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema kikosi chake kinahitaji kushinda mchezo wa kesho dhidi ya Mtibwa Sugar bila ya kujali mazingira watakayok-kutana nayo
Simba iliwasili mkoani Morogoro jana ambapo leo itakamilisha maandalizi yake kuelekea mchezo huo utakaopigwa uwanja wa Jamhuri
Mazingira ya uwanja hayakumfurahisha Sven kwani atalazimika kubadili mbinu zake kwa kuwa soka la pasi fupifupi halitawezekana kwenye uwanja huo
Hata hivyo Sven amesema hiyo haiwezi kuwa sababu ya kuwafanya washindwe kupata ushindi kwenye mchezo huo
"Hakuna sababu iwe ni hali ya uwanja, mvua, jua au waamuzi wa mchezo kesho haipaswi kuwa sababu. Ni ushindi pekee ndio tunahitaji na tuna kazi ya kuhakikisha tunafanikisha hilo," amesema Sven
Vinara hao wa ligi kuu wanahitaji kushinda mchezo huo ili kurejesha furaha ya mashabiki wao ambao walichukizwa na matokeo ya kufungwa mchezo uliopita