Mshambuliaji mpya wa Yanga David Molinga 'Falcao' juzi kwenye mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi dhidi ya Kariobangi Sharks alicheza kwa takribani dakika tano tu
Hata hivyo wapo waliotumia dakika hizo tano, kumuhukumu
Molinga hakuwa kwenye mpango wa kocha Mwinyi Zahera katika mchezo huo kwa kuwa hakuwa amefanya mazoezi na wachezaji wengine
Hata hivyo alimpa nafasi ili kuwapa fuhara mashabiki ambao walikuwa na shauku ya kumuona
Molinga yuko Zanzibar akijifua na kikosi cha Yanga kinachojiandaa na mchezo dhidi ya Township Rollers
Hakuna shaka atakapokuwa ameiva, kazi yake itaonekana uwanjani
Lakini dakika tano alizocheza juzi hazitoshi kusema ni mchezaji wa aina gani
ADVERTISE HERE